Home AJIRA Unatafuta kazi mpya? Fahamu haya

Unatafuta kazi mpya? Fahamu haya

0 comment 156 views

Sio vibaya kutafuta kazi nyingine ikiwa umeajiriwa. Ili kuweza kukua ni vyema kubadilisha mazingira ya kazi kila baada ya muda ili kujipatia ujuzi  na uzoefu zaidi. Maamuzi ya kuacha kazi yako ya sasa na kwenda kutafuta kazi nyingine yanaweza kuleta faida au migogoro zaidi kuliko ile ambayo umekuwa ukipitia katika kazi yako ya sasa.

Watu wengi wameacha kazi zao sababu ya mazingira magumu na kupata kazi zenye mazingira magumu zaidi, hivyo ni muhimu kutafakari na kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kuamua kufanya mabadiliko katika swala zima la ajira yako. Hivyo basi, nini cha kufanya ili kupunguza hatari ya kufanya harakati au maamuzi kuhusu kazi?

Ni vizuri kufanya mabadiliko, lakini kabla ya kuyafanya mabadiliko hayo ni muhimu kuangalia hali yako katika mtazamo mwingine ili kujua kama kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko hayo. Pia angalia unataka kufikia wapi katika malengo yako na kama kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko katika kazi yako ili kuweza kuyafikia malengo  hayo. Aidha, fahamu tabia ambazo utahitaji kuwa nazo ili kuweza kufanikiwa na weka mfumo wa kuzifanya tabia hizo kila siku.

Watafuta kazi wengi huanza kutafuta kazi huku wakizingatia vigezo visivyo sahihi. Mara nyingi huwa wanaorodhesha vitu kama mshahara bora, faida, sehemu ya kazi nk. Ni kweli kuwa mambo hayo ni muhimu na yanapaswa kuainishwa, lakini vigezo vifuatavyo ni muhimu zaidi kuzingatia wakati unatafuta kazi:

Je, kazi unayotaka kuifanya inatatua shida unayojali?

Katika ulimwengu wa sasa ni muhimu kufanya kazi ambayo ina kusudi. Tunapoamini kazi zetu zina maana ni rahisi kurizika na kushiriki kikamilifu katika kazi husika hivyo kupelekea uzalishai wa hali ya juu na mafanikio. Kama kazi unayoifanya au unayotaka kufanya haichangii katika kitu au mambo unayoyajali itakuwa ngumu kupata motisha ya kufanya kazi hiyo. Hivyo ni muhimu kujua uhusiano wa kazi unayotaka kuifanya na athari (nzuri au mbaya) zinazotokana na kazi hiyo. Watu wengi wamefanikiwa kutokana na kufanya kazi wanazofurahia kufanya pamoja na kazi zinazoleta maana na kugusa katika mambo wanayoyajali zaidi.

Je, utatumia njia unazopendelea kufanya kazi?

Ni dhahili kuwa kila mtu ana ujuzi na uwezo mwingi lakini haimaanishi kuwa tunataka kutumia ujuzi wote kila siku. Ikiwa utaelewa jinsi unavyotaka kutekeleza majukumu na kuunda thamani kwa muajiri basi itakurahisishia mchakato wako wa utafutaji wa kazi. Ni muhimu kujua kuwa kila kampuni huhitaji ujuzi wa aina tofauti tofauti ili kuweza kufikia malengo ya kampuni hivyo ni muhimu kujua ni ujuzi gani unaweza kutumia katika kampuni ipi ili kurahisisha swala zima la mabadiliko yako katika upande wa kazi.

Pia ni muhimu kutengeneza orodha kuhusu mahojiano ili kuweza kuelewa hali yako, na nafasi uliyo nayo katika kuipata kazi husika. kuwa na uelewa kuhusu kampuni husika na bidhaa au huduma wanauza kutawafanya watu wanaokuhoji wakati wa usaili kuona kuwa unajali kuhusu kampuni yao, upo tayari kuleta mabadiliko katika kampuni yao na uko makini.

 

 

Tags:

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter