Home AJIRA Wafanyakazi hawafurahii vitu hivi

Wafanyakazi hawafurahii vitu hivi

0 comment 93 views

Siku zote wafanyakazi katika kampuni wakiwa na furaha basi shughuli katika biashara au kampuni hiyo huendelea vizuri. Mmiliki wa biashara au kampuni ana jukumu la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wake wana furaha ili mambo yaende sawa kwa sababu kutokuwa na furaha kwa wafanyakazi kunaweza kusababisha shughuli isiendelee, na mwisho wa siku kushindikana kabisa na kupelekea kuifunga shughuli hiyo.

Hivyo ikiwa wafanyakazi wako wanaonyesha kutokuwa na furaha basi chunguza yafuatayo ili kupata suluhisho na kuwarudisha katika mstari:

Malipo madogo, Ikiwa wafanyakazi wanaonyesha kutofurahishwa kufanya kazi katika biashara au kampuni yako basi anagalia mfumo wako wa malipo kwa ujumla. Hivyo angalia kiasi unachowalipa na kazi wanayofanya baada ya kuangalia hilo basi fikiria namna utakavyoweza kuwaongezea mshahara kwamfano unaweza kupunguza matumizi yasiyo na umuhimu ili kuongeza fedha kwenye mishahara ya wafanyakazi wako.

Hata wafanyakazi wana haki ya kupewa muda wa kupumzika kidogo ili aweze kupata nguvu zaidi na wakati mwingine kuweza kutatua mambo yao. hivyo ikiwa hufanyi hivyo ni dhahiri wafanyakazi wako watakuwa wanashindwa kufanya mambo yao binafsi hivyo hawatafurahia sana hii inaweza kusababisha watu waache kazi kwa sababu muda wote wako kazini na wanashindwa kufanya shughuli nyingine. Hivyo weka utaratibu kwa kila mfanyakazai kujipatia muda kidogo wa kukabiliana na mambo mengine.

Wafanyakazi hususani vijana hufurahi zaidi kama ofisini au sehemu ya biashara kazi zikifanywa katika mienendo ya kidigitali. Hivyo ikiwa unang’ang’ania mifumo ya kizamani katika utendaji wa kazi basi tegemea wafanyakazi wengi kutokufanya kazi zao ipasavyo kwani watafanya kwa manunguniko ili hali wanajua kuna njia za kisasa ambazo zinaweza kuwasaidia kufanya kazi hiyo hiyo bila shida yoyote. Hivyo tengeneza mahusiano mazuri na wafanyakazi wako, wape nafasi ya kutoa maoni yao, wasifie wakifanya kazi vizuri ili kuwapa motisha ya kufanya mambo makubwa zaidi.

Aidha wafanyakazi hawawezi kuwa na furaha ikiwa bosi wa kampuni au biashara husika hatilii maanani nafasi walizonazo wafanyakazi wake katika kampuni. Kuonyesha unajari uwepo wa kila mfanyakazi kutaepusha mawazo ya upendeleo baina ya wafanyakazi na kutawasaidia wafanyakazi kufanya kazi kwa usawa na kwafuraha.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter