Benki ya CRDB leo Novemba 06 imezindua kampeni maalumu inayolenga kusogeza huduma karibu zaidi na wateja ijulikanayo kama “Tupo Mtaani Kwako”.
Taarifa iliyotolewa na benki ya CRDB inasema kupitia kampeni hii wateja watapata elimu na ushauri juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na benki.
Pia wateja wataweza kuunganishwa na huduma za benki ikiwemo kufungua akaunti na kuweka akiba papo hapo.
CRDB imesema kampeni hiyo itawawezesha wateja wake kupata elimu juu ya njia mbadala za upatikanaji wa huduma za CRDB Wakala, SimBanking, Internet banking na SimAccount.