Kuelekea Mkutano Mkuu wa wanahisa, Benki ya CRDB imeendesha semina ya elimu ya fedha na uwekezaji kwa wanahisa wake.
Semina hiyo, ambayo imefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), imehudhuriwa na watu zaidi ya 2,000 ambapo Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba alikuwa mgeni rasmi.
Katika semina hiyo, mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo elimu ya fedha na uwekezaji, biashara ya hisa kidigitali, huduma ya bima ya maisha (KAVA Assuarance) pamoja na fursa za uwekezaji kupitia CRDB Wakala.