Home BENKI Hatifungani ya kijani yavuka lengo

Hatifungani ya kijani yavuka lengo

0 comment 122 views

Hatifungani ya kijani ya benki ya CRDB imevuka lengo lililokusudiwa la shilingi bilioni 40 kwa asilimia 329.55 ikiwa ni awamu ya kwanza ya uuzwaji.
Benki ya CRDB imetangaza rasmi matokeo ya hatifungani hiyo iliyouzwa kwa siku 38 kuanzia Agosti 31, 2023.

Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikua ni Dkt. Charles Mwamwaja, Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha wa Wizara ya Fedha aliemuwakilisha Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza Benki ya CRDB kwa mafanikio hayo kwani fedha zilizokusanywa zitasaidia kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo na yenye faida nyingi za kimazingira kwa wananchi na taifa kwa ujumla, kutoa ajira kwa vijana na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ameelezea kuwa matokeo haya ni kiashirio cha imani walionayo wawekezaji wa ndani pamoja na nje ya nchi.

“Matokeo haya tuliyopata yanaendelea kuifanya Benki yetu kuwa na uwezo wa kufanikisha miradi inayolenga kulinda mazingira, ameeleza Nsekela.

Ameshukuru kwa kazi nzuri inayofanywa na Serikali katika kuimarisha uchumi wa nchi kwani Benki isingeweza kufikia makafanikio hayo endapo hali ya ukwasi katika soko isingekua ya kuridhisha.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter