103
Benki Kuu ya Tanzania ni benki ya kiserikali inayojihusisha na utoaji wa huduma za kifedha kwa serikali na taasisi binafsi za kifedha, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa sera za kifedha na utoaji wa sarafu
Yafuatayo ni majukumu makuu ya Benki Kuu katika kukuza uchumi wa taifa:
- Benki kuu ina jukumu la kusimamia na kutathmini utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga kuwa na kiwango kidogo cha mfumuko wa bei kwa ajili ya ukuaji endelevu wa pato la taifa.
- Kusimamia na kufanya tathmini kuhusu matokeo ya sera ya fedha kwenye uchumi na kutoa ushauri wa kisera kwa benki na serikali, ili sera ziendane na hali halisi ya uchumi.
- Kukusanya na kuchambua takwimu za urari wa malipo na kutoa ushauri kwa benki juu ya sera ya fedha za kigeni, na pia kutoa ushauri stahiki kwa serikali juu ya sera za kuboresha uhalali wa malipo.
- Kukusanya na kuchambua takwimu za mapato na matumizi ya serikali na kutoa ushauri kwa serikali.
- Kutunza takwimu na madeni ya sekta binafsi na ya serikali ili kuhakikisha kuwa deni la nchi ni endelevu.
- Kuandaa sera ya ukuzaji masoko madogo madogo ya fedha (Microfinance)
- Kuimarisha uhusiano wa karibu na taasisi za fedha za kimataifa na kushiriki katika majadiliano ya sera kati ya serikali na vyombo vya fedha vya kimataifa.
- Kufuatilia maendeleo ya uchumi wa dunia na kutathmini matokeo yake katika shughuli za kiuchumi nchini.