Home BENKI MAMBO AMBAYO BENKI HAWATAKI MTEJA UJUE

MAMBO AMBAYO BENKI HAWATAKI MTEJA UJUE

0 comment 107 views

Ni muhimu kutunza fedha kwa ajili ya matumizi ya siku za baadae. Benki ni moja ya sehemu salama za kutunza fedha. Ieleweke kuwa sisi tunazihitaji benki na benki zinatuhitaji sisi. Kutokana na hilo kuna baadhi ya mambo ambayo benki nyingi huwa haziwaelezi wateja wao.

Baadhi ya mambo hayo ni:

-Sio mara zote wakopaji waliothibitishwa hupata viwango sawa. Benki hutoa viwango vya chini kwa baadhi ya watu waliothibitishwa na huku wengine waliothibitishwa hutakiwa kulipa viwango vikubwa zaidi. Hivyo ikiwa unatakiwa kukopa unatakiwa kujua kuwa unaweza kuongea na benki kuhusu viwango walivyotangaza na kupatana nao kuhusu punguzo.

-Pale unapotumia kadi yako kununua bidhaa au huduma katika maduka yenye mashine za kuwezesha kutumia kadi, siku zote mwenye duka hutozwa ada kwa ajili ya kuwezesha shughuli hiyo ambapo ada hiyo hurudi katika benki yako. Hivyo benki hupata faida zaidi bila wewe kujua.

-Ikiwa unataka kukopa, benki wataangalia historia yako ya ukopaji. Katika hali ya kawaida mtu asiye na madeni huonekana kuwa ndio mtu makini sana, lakini hiyo ni tofauti kwa benki yoyote. Huwezi kupewa mkopo kama huna historia ya kukopa, kwa sababu benki haijui wewe ni mkopaji wa aina gani, benki nyingi ziko tayari kumkopesha mkopaji asiye na historia ya kuridhisha sana kuliko mkopaji wa mara ya kwanza.

ADVERTISEMENT

-Siku zote mkopaji hujitahidi kutafuta fedha na kulipa mkopo wake mapema. Ikiwa umekopa katika benki basi jua kuwa kitendo cha kuwahi kulipa mkopo wako hupelekea kulipa malipo ya ziada. Hivyo sio lazima kuwahi kulipa mkopo lakini hakikisha unalipa kutokana na wakati mliokubaliana.

-Benki huwaeleza wateja wake kuwa kuna baadhi ya miamala ni bure au kufungua akaunti ni bure, hakuna malipo ya ziada. Hii si kweli, hakuna vitu vya bure. Kwa namna moja ama nyingine tunalipia vitu vya bure.

Hivyo ni muhimu kuuliza maswali katika benki yako ili kujua mambo yanaendaje, ili kujua njia mbadala ambazo zitapunguza makato yasiyo na umuhimu katika akaunti yako.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter