Home BENKI NMB yapongezwa kuunga mkono wajasiriamali

NMB yapongezwa kuunga mkono wajasiriamali

0 comment 82 views

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Mohammed Ahmada amepongeza mchango wa benki na taasisi za fedha kwa ujumla katika kuinua biashara za wajasiriamali. Naibu Waziri Ahmada amesema hayo wakati akifungua mkutano wa mafunzo kwa wanachama wa klabu ya biashara ya benki ya NMB Zanzibar (NMB Business Club) na kuongeza kuwa, kupitia mafunzo wanayopewa wajasiriamali takribani 300 na benki hiyo, watapata uzoefu wa masuala ya kodi.

“Katika hili hata pale mteja anapokosa nafasi ya kwenda benki kuelimishwa jambo linalohusu biashara au mabadiliko, ataweza kupata elimu hiyo kupitia wanachama wenzake na hivyo kukuza uelewa wa biashara na masuala ya benki”. Amesema Ahmada.

Aidha, ameshukuru benki hiyo kwa kuandaa mkutano huo ambao utawanufaisha wajasiriamali kuhusu namna bora ya kutunza kumbukumbu za biashara, masoko, huduma kwa wateja, upangaji bei, sheria za biashara na mahesabu na elimu ya kodi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Biashara NMB, Donatus Richard amesema klabu hiyo ilianzishwa mwaka 2012 na kuanza na wanachama 50. Kwa Zanzibar, ilianza mwaka 2015  na hadi sasa ina wanachama zaidi ya 300.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter