Home BENKI Stanbic yazindua soko la fedha mtandaoni

Stanbic yazindua soko la fedha mtandaoni

0 comment 123 views

Benki ya stanbic imezindua huduma ya soko la fedha za kigeni utakaoruhusu mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni mtandaoni uitwao ‘eMarket Trader’ ambao utawapatia wateja huduma mahsusi ya kubadilisha fedha za kigeni ikiwemo kujua taarifa za thamani ya fedha za kigeni na mwendo wa soko kwa wakati husika.

 

Huduma hiyo ambayo inajumuisha wateja binafsi na makampuni ni ya kwanza nchini Tanzania na wateja wanaweza kubadilisha fedha zao kwa urahisi kwa kuwapatia aina tofauti tofauti zaidi ya 64 za fedha za kigeni zilizopo sokoni katika muda husika.

 

Hafla hiyo ya uzinduzi ilihudhuliwa na wageni mbalimbali akiwemo meneja masoko na fedha kutoka Benki kuu ya Tanzania (Bot) Bwana Lameck Kakulu ambaye alisema “Tunafurahi kwa benki ya stanbic ambao ni moja ya wadau muhimu katika sekta ya fedha nchini wakkijikita zaidi katika teknolojia,kupitia uboreshaji huu wenye vipengele muhimu vya kidigitali vinavyomuwezesha mteja kupata taarifa za soko katika muda halisi na upatikanaji wa tafiti za benki ya standard benki”.

 

Pia mkuu wa kitengo cha fedha za kigeni benki ya stanbic Bw Erick mushi alisema kuwa haina haja ya kupiga simu kitengo cha ubadilishaji fedha kwa ajili ya kununua au kuuza fedha zao bali kupitia eMarket Trader wateja wanaweza kupata taarifa zote na kubadilishha fedha kwa wakati.

 

Biashara ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni biashara inayokua kwa kasi nchini ambapo matumizi ya teknolojia yamekua ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha huduma hizi zinakua rahisi na zinafika kwa wananchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter