Home BENKI TIRA yazindua kanuni za bima kupitia benki

TIRA yazindua kanuni za bima kupitia benki

0 comments 162 views

Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zimezindua Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations).

Akizindua rasmi kanuni hizo Jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Yamungu Kayandabila amezitaka taasisi za fedha na benki nchini kuzizingatia katika utoaji wa huduma zao ili kuongeza ufanisi wa shughuli zao.

Alisema kanuni hizo zitasaidia kusambaza huduma ya bima nchini kwani watu wengi bado hawajafikiwa. “Ujio wa Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki nchini Tanzania umechelewa kidogo hivyo wadau wana kila sababu ya kuzingatia kwa manufaa ya pande zote watoa huduma na wanufaika,” alisema.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dr Yamungu Kayandabila akizungumza wakati wa uziduzi wa rasmi Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema endapo wadau watazizingatia kanuni hizo mapato katika sekta hiyo kiujumla yataongezeka kwa taifa, watoa huduma na watu wengi zaidi watafikiwa na huduma za bima.

Aidha kwa upande wake akizungumza katika hafla hiyo alisema licha ya manufaa lukuki ya uzinduzi wa kanuni hizo pia unalenga kuendeleza ajenda ya TIRA ya kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za bima nchini yaani bima kwa wote.

“Tunahitaji kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za Bima (access) nchini kwa kuongeza aina mbalimbali za bima kwa mahitaji mbalimbali, mfano mbadala wa uuzaji na usambazaji wa huduma za bima ikiwemo kutumia benki,” alisema Kamishna huyo aliongeza kuwa inahitajika teknolojia rahisi na rafiki kwa ajili ya kusambaza bima, kununua bima, kuuza bima, kulipa mafao/madai ya bima, kusikiliza maoni na mahitaji ya wananchi, kuchakata na kuandikisha maombi ya bima,” alisema Dk. Saqware.

Kamishna wa TIRA, Dk. Baghayo Saqware akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations) uliofanyika jijini Dar es Salaam

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa kanuni hizo ni muhimu katika kuendeleza sekta ya kifedha nchini na kusisitiza kuwa pato la taifa, hasa ukizingatia faida nyingi ambazo zitapatikana kwa benki zenyewe na watumiaji wa huduma za bima.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali serikalini, makampuni ya bima, taasisi za kifedha, mawakala mbalimbali na wadau wa sekta ya bima na kudhaminiwa na BoT, Reliance Insurance, Heritage Insurance, Zanzibar Insurance, Chama Cha Watoa Huduma za Bima (ATI), NMB, CRDB Insurance, Metropolitan Life Tanzania, Jubilee Insurance, FSDT, Stanbic Bank, Smart Policy, Alliance Insurance, TPB Bank na Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Baadhi ya wadau waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!