Home BIASHARA Akaunti ya benki muhimu kwa biashara

Akaunti ya benki muhimu kwa biashara

0 comment 153 views

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa wafanyabiashara au wajasiriamali kutumia fedha za biashara katika mambo binafsi au kufanya miamala katika akaunti zao za biashara kulipia mambo binafsi, jambo ambalo lazima lilete athari kwa namna moja au nyingine katika pande moja au pande zote mbili.

Hata hivyo, zipo sababu mbalimbali ambazo zinaeleza ni kwanini unapaswa kutenganisha fedha zako za biashara na fedha zako binafsi. Kuwa na akaunti ya biashara kutatenganisha mali zako binafsi, na kufanya upate rekodi nzuri ya masuala ya ushuru.

Zifuatazo ni sababu zinazoeleza umuhimu wa kufungua akaunti ya biashara:

Wafanyabiashara wengi wadogo huunda dhima ndogo (Limited Liability Company-LLC)  au ushirika ili kulinda mali binafsi na matatizo yanayoweza kuitokea biashara kwamfano biashara ikiwa ina kesi ya madai,au mikopo. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa una akaunti ya benki ya biashara na mambo yako binafsi hayaingiliani na yale ya biashara kwa namna yoyote kwa sababu muingiliano wowote unaweza kuathiri pande zote mbili.

Mara nyingi watu wana kawaida ya kukopa kwa ajili ya biashara na kuwekeza nyumba wanayoishi, ikiwa mhusika ameshindwa kulipa mkopo husika basi benki huwa na kila mamlaka na haki ya kuuza nyumba au mali ya mkopaji ili kujilipa fedha zao, sasa hii si nzuri sana kwa sababu huleta changamoto kubwa katika biashara na maisha binafsi.

Akaunti ya benki ya biashara humsaidia mfanyabiashara kuwa na mfumo mzuri wa nyaraka za kumbukumbu ikiwa inahitajika kukaguliwa masuala ya kodi. Kuchanganya matumizi binafsi na ya biashara kutafanya utumie muda mwingi kutofautisha nyaraka za kumbukumbu za matumizi ya fedha.

Wateja hufurahishwa zaidi na huduma zinazofanyika kitaalamu. Kuwa na akaunti ya biashara kutawahikikishia wateja wako kuwa uko makini na biashara yako na mambo yanafanyika kitaalamu.

Benki ni nyingi na kila benki ina masharti na vigezo vyake vya kumruhusu mtu afungue akaunti binafsi au ya biashara. Wamiliki wa biashara wanapaswa kutathmini ukubwa wa biashara yako na kujua taarifa kamili kuhusu benki husika ikiwa ni pamoja na masharti, mikopo n.k kwani baadhi ya benki huhitaji vitu kama ‘notice’ ikiwa unataka kutoa kiasi kikubwa cha fedha hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kufanya utafiti wa kina.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter