Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Fanya biashara hizi kwa mtaji mdogo tu

Fanya biashara hizi kwa mtaji mdogo tu

0 comment 290 views

Ajira bado ni tatizo kubwa hapa nchini hasa kwa vijana. Wengi wamelazimika kufikiria mbinu nyingine za kutengeneza kipato ili waweze kumudu gharama za maisha. Kikwazo kikubwa ambacho wajasiriamali wengi wamekuwa wakikutana nacho ni kukosa mtaji wa kuanzisha biashara. Kuokana na hili, wengi wamekwama japokuwa wamefikiria mawazo mazuri ya biashara.

Siku hizi kuna biashara ambazo uendeshaji wake unahitaji gharama kidogo tu kulingana na mazingira yanayokuzunguka. Unaweza kufanya utafiti na kutambua fursa zinazokuzunguka. Baadhi ya biashara ambazo zinaweza kufanyika kwa mtaji wa mtaji mdogo kuanzia laki mbili (200,000) ni hizi:

1. Kuuza nguo
Biashara hii inawezekana kwa mtaji kidogo tu. Mfanyabiashara wa nguo anatakiwa kwenda kwenye masoko makubwa ya nguo na kuchagua nguo nzuri na kisha kuuza maeneo ya mitaani. Kadri unavyopata nguo nzuri na jinsi unavyoweza kuwa na kauli nzuri ndivyo unavyoweza kufanya mauzo makubwa. Ni muhimu kuongea vizuri na watu. Nguo za wanawake na watoto zina soko kubwa zaidi hivyo unaweza kuanzia hapo.

2. Kuuza mboga mboga au matunda
Biashara nyingine ambayo mtu anaweza kuanza kwa mtaji kidogo ni hii ya mboga mboga au matunda. Haya ni mahitaji ya msingi ambayo huhitajika kila siku hivyo kama unaweza kupata bidhaa zilizo bora na kuuza kwa bei nzuri, unaweza kutengeneza biashara ambayo itazalisha faida lukuki.

3. Huduma za maji safi
Kuna maeneo mengi hususani katika jiji la Dar es salaam ambapo watu bado hawapati huduma ya maji safi na salama au labda huduma hiyo inapatikana mbali na makazi yao hivyo wengi kushindwa kuyapata. Unaweza kutumia fursa hiyo kuwasambazia watu maji masafi. Unahitaji kuwa na usafiri wa uhakika ili kufikisha maji eneo husika, kufahamu wapi utapata maji safi na kuweza kuwasambazia wateja wako na vilevile kuwa tayari kutoa huduma muda wowote itakapohitajika.

Unapoanza biashara kwa mtaji kidogo, unapaswa kutambua kuwa unakosa uhuru mkubwa wa kuchagua aina fani ya biashara unataka kufanya. Hapa unahitaji kufanya biashara yoyote ambayo inaweza kuzalisha faida mapema. Ukishapata biashara ya aina hii, wekeza jitihada zako zote mpaka pale biashara inapoimarika na kukupa uhuru wa kuanza kufanya kile ambacho unapenda.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter