Home BIASHARA Wapandisha bei msimu wa Ramadhan waonywa

Wapandisha bei msimu wa Ramadhan waonywa

0 comment 76 views

Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Joseph Abdallah Meza ametoa onyo kwa wafanyabiashara wenye mazoea ya kutumia mfungo wa Ramadhan kupandisha bei kiholela ili kujiongezea kipato. Kamishna huyo amedai imekuwa kawaida kwa wafanyabiashara kuwa na tamaa na kupandisha bei ovyo hali ambayo imekuwa inawapa shida wananchi.

Ameongeza kuwa bidhaa zinazopanda bei ni zile zinazozalishwa ndani ya nchi na bodi hiyo inaandaa mkakati wa kupunguza ushuru kwa bidhaa zenye uhitaji mkubwa zaidi kipindi cha mwezi mtukufu kama vile tende na tambi.

Kwa upande wao, baadhi ya wafanyabiashara wamejitetea kuwa wanalazimika kupandisha bei kutokana na gharama wanazotumia katika ununuzi na usafirishaji kupanda huku wengine wakisema inawalazimu kuongeza bei baada ya wakulima nao kupandisha bei zao.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter