Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Serikali ya Tanzania kuwakopesha boti wavuvi

Serikali ya Tanzania kuwakopesha boti wavuvi

0 comment 147 views

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amesema serikali ina mpango wa kununua boti 320 kwa nchi nzima ili kuwakopesha wavuvi wadogo na wavuvi wa kati. Mikopo ya Wavuvi

Waziri amesema lengo ni kuwaweze wavuvi hao kuvua kwenye maji marefu upande wa bahari lakini pia upande wa maziwa.

Akijibu swali Bungeni jijini Dodoma Waziri amesema boti hizo zitanunuliwa kwenye bajeti ya mwaka ujao na kuzikopesha kwa wavuvi kwa nchi nzima.

Ameeleza kuwa “tuna mpango wa kuboresha mialo na kuijenga katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha masoko madogo madogo ya wavuvi kwa kujenga vichanja ili mazao yanayotolewa baharini au ziwani yaweze kuanikwa vizuri na kuwa bora ili kupata bei nzuri sokoni”.

 

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter