Home BIASHARA Fanikisha biashara nyumbani kwa kuzingatia haya

Fanikisha biashara nyumbani kwa kuzingatia haya

0 comment 101 views

Wafanyabiashara wanaofanyia biashara zao nyumbani huwa wanakuwa na uhuru wa kufanya biashara hizo muda wowote, hivyo hupata muda wa kufanya shughuli nyingine huku wakiendelea kujipatia fedha. Kutokana na hilo, mfanyabiashara anatakiwa kuwa makini na uhuru huo kwa sababu biashara yake inatakiwa kuwa na mpangilio mzuri ili iweze kuzaa matunda na sio vinginevyo.

Mambo ya kuzingatia:

  • Panga muda wako vizuri: Ili mambo yaende katika biashara yako unatakiwa kupanga muda vizuri, usichanganye mambo ya nyumbani na mambo yanayohusu biashara yako. Mfanyabiashara anatakiwa kuthamini biashara yake kwa sababu kwanza hiyo ni ofisi yake pili yeye ndio atakayefaidika ikiwa biashara hiyo itazaa matunda na ikiwa atapata hasara yeye ndio itamuathiri. Hivyo ni muhimu kutenga muda wa kazi na muda wa mambo binafsi.
  • Tengeneza mazingira mazuri ya kazi: Kufanyia biashara nyumbani isiwe sababu ya kufanyia kazi zako katika mazingira yasiyoeleweka. Kwa kufanya hivyo hata wewe utakuwa hauna umakini stahiki katika shughuli zinazohusu biashara hiyo. Hivyo tengeneza mazingira mazuri, masafi, yanayokuridhisha na kama mteja atafika nyumbani kwako kwa ajili ya kununua bidhaa au huduma basi avutiwe na mazingira ya nyumbani kwako.
  • Tengeneza tovuti na akaunti mbalimbali: Tofauti na zamani, siku hizi mambo mengi yanafanyika mtandaoni ikiwa ni pamoja na masuala ya biashara. Hivyo ili kujipatia wateja wengi tengeneza tovuti (zinapatikana kwa bei tofauti tofauti angalia unayoweza kulipia) na akaunti mbalimbali katika mitandao ya kijamii. Jambo la muhimu kwenye tovuti na mitandao mbalimbali ni kuwa mkweli kuhusu bidhaa unazouza au huduma. Hivyo weka taarifa, picha n.k za ukweli kuhusu bidhaa au huduma yako.
  • Muonekano wako ni muhimu pia: Kufanyia biashara nyumbani isiwe sababu ya kutojali muonekano wako. Hivyo jitahidi kuvaa vizuri kama mtu ambaye anaenda kazini kwake kwa sababu biashara yako ni kazi yako. Kuwa nadhifu siku zote huleta hamasa ya kutekeleza yako kwa bidii zaidi.

Aidha, unatakiwa kukumbuka kila siku kuwa hakuna mtu ambaye ataijali biashara yako kama ambavyo wewe utaijali. Hivyo jua vipaumbele vyako na fanya kila jitihada kutimiza malengo ya biashara yako.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter