172
Dhahabu ni elementi yenye namba atomia 79 katika mfumo radidia na uzani atomia ni 196.966569. Alama ya madini hayo ni Au inayotokana na neno la kilatini aurum.
Je, Wajua:
- Dhahabu ni madini pekee yenye rangi ya njano kwa asili, ingawa madini mengine yanaweza kubadilika rangi na kuwa na unjano lakini hii huwa inatokea ikiwa madini hayo yamechanganywa na kemikali.
- Dhahabu ilikuja duniani kutokana na Asteroidi iliyodondoka duniani kujitengeneza zaidi ya miaka 200 iliyopita.
- Alama ya dhahabu ni Au. Inayotokana na jina la kale la kilatini dhahabu aurum, ambalo linamaanisha “kuangaza alfajiri” au “mwanga wa jua.” Neno dhahabu linatokana na lugha ya kijerumani, inayotokana na Proto-Germanic gulþ na Proto-Indo-European ghel, lenye maana “njano / kijani.” Elementi hii imeanza kujulikana tangu zama za kale.
- Ounce moja ya dhahabu (juu ya gramu 28) inaweza kuunganishwa na kufikia urefu wa kilomita 8 za dhahabu. Hivyo uzi wa dhahabu unaweza kutumika kushonea.
- Karatasi ya dhahabu inaweza kufanywa nyembamba kiasi cha kuonyesha upande mwingine. Karatasi nyembamba sana la dhahabu linaweza kuonekana la rangi ya bluu au kijani kwa sababu gold huakisi rangi ya njano au nyekundu.
- Kuna aina ya dhahabu laini ambayo inaweza kuliwa au kuwekwa kwenye vinywaji
- Dhahabu kamili haina harufu wala ladha.
- Dhahabu kamili (Pure gold) ina karati 24, na dhahabu yenye karati 18 huwa ni asilimia 75 ya ukamilifu wake (Pureness), huku karati 14 huwa ni asilimia 58.5 ya dhahabu safi.
- Dubai kuna mashine ya ATM kwaajili ya kutoa dhahabu.
- Inaelezwa kuwa kipande kikubwa zaidi cha dhahabu duniani kina kilo 250. Kipande hicho kinamilikiwa na kampuni ya Mitsubishi, na kinakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Marekani 3,684,000.
Kwa ujumla dhahabu inapatikana katika kila bara duniani, na thamani yake haijawahi kushuka. Kila kona duniani, watu hufanya jitihada kubwa kupata dhahabu ili waweze kutajirika.