Home BIASHARA PAC:Hatujafurahishwa na wafanyabiashara kuhama TPA

PAC:Hatujafurahishwa na wafanyabiashara kuhama TPA

0 comment 108 views

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka amesema kamati hiyo haijafurahishwa na matukio ya wafanyabiashara wakubwa kuihama Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na kutoa wito kwa serikali kuangalia uwezekano wa kurekebisha baadhi ya sheria. Kaboyoka amesema hayo wakati PAC ikiihoji mamlaka hiyo kuhusu utekelezaji wa maagizo ya kufanya tathmini ya mali kama ilivyoagizwa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na kujibu hoja zilizoibuliwa mwaka 2016/2017.

Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa kuna kila sababu ya sheria zilizopo kufanyiwa maboresho ya maana kwani pasipo kuchukua tahadhari, bandari hiyo haitofika mbali. Pamoja na hayo, Kaboyoka ameongeza kuwa ili kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa watapeleka ripoti itakayoonyesha changamoto zote zilizopo ndani ya TPA ili mabadiliko yafanyike na wafanyabiashara warudi kama ilivyokuwa hapo awali.

“Kamati haikufurahishwa na wafanyabishara wakubwa kuhama na ina changamoto na imefungamana na sheria zilizopitishwa na bunge, hivyo inabidi ziangaliwe upya na kuboreshwa”. Ameeleza Mwenyekiti huyo.

Kuhusu mapato ya mamlaka hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka amesema mapato yameongezeka kutoka Sh. 734 bilioni kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 hadi Sh. 838 kwa mwaka 2017/2018.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter