• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Thursday, March 30, 2023
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Ubelgiji yatakiwa kuongeza uwekezaji nchini

“Kuna miradi 32 yenye thamani ya Euro milioni 902 ambayo imeajiri wafanyakazi 1814 inayomilikiwa na wawekezaji kutoka Ubelgiji nchini Tanzania. Hivyo, kuna umuhimu wa kuongeza uwekezaji huo kwa kuwa mazingira ya uwekezaji nchini ni mazuri na yanavutia”, Mhandisi Manyanya alisema.

Patricia Richard by Patricia Richard
October 26, 2018
in UWEKEZAJI
0
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga (kulia) pamoja na wafanyabiashara kutoka Ubelgiji wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri Manyanya.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga (kulia) pamoja na wafanyabiashara kutoka Ubelgiji wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri Manyanya.

Share on FacebookShare on Twitter

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ubelgiji yaambiwa iongoze uwekezaji nchini, Mhandisi Manyanya

Ubelgiji imetakiwa kuongeza kiwango cha uwekezaji nchini ili kuchochea zaidi kasi ya azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Wafanyabiashara wa Ubelgiji na Tanzania linalofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

“Kuna miradi 32 yenye thamani ya Euro milioni 902 ambayo imeajiri wafanyakazi 1814 inayomilikiwa na wawekezaji kutoka Ubelgiji nchini Tanzania. Hivyo, kuna umuhimu wa kuongeza uwekezaji huo kwa kuwa mazingira ya uwekezaji nchini ni mazuri na yanavutia”, Mhandisi Manyanya alisema.

Mhe. Naibu Waziri aliwahamiza wawekezaji hao ambao ni wafanyabiashara wakubwa nchini Ubelgiji kuwekeza katika sekta za kilimo, hususan kwenye maeneo ya viwanda vya nguo, sukari, mafuta ya kupikia, maziwa, ngozi, nyama, mbegu, matunda na maua. Sekta nyingine aliyoitaja ni ya nishati hasa katika miundombinu ya kuzalisha na kusambaza gesi asilia na nishati jadilifu.

ADVERTISEMENT

Maeneo mengine yaliyosisitizwa na Mhe. Naibu Waziri ni pamoja na sekta ya utalii, madini, uvuvi katika bahari kuu, miundombinu, maeneo maalum ya viwanda (industrial parks) na ujenzi wa majengo hususan katika mji
mkuu wa Dodoma ambapo mahitaji ni makubwa.

Uzalishaji wa dawa za binadamu na wanyama, vifaa tiba na uzalishaji wa samani za kisasa ni maeneo ambayo Mhe. Naibu Waziri aliwasihi wawekezaji hao kuyapa jicho la pekee.

Mhe Manyanya alisema wawekezaji watakaoamua kuwekeza nchini hawatajutia uamuzi wao kwa kuwa Tanzania kuna mazingira mazuri. Mazingira hayo ni pamoja na amani na usalama, rasilimali za kutosha na uhakika
wa soko kwa kuwa Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika na hatua zinakamilishwa kuwa na eneo huru la biashara barani Afrika.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mathew Mnali aliwahakikishia wawekezaji hao kuwa TIC itatoa msaada unaohitajika kupitia kituo chake cha
kutoa huduma kwa pamoja (One Stop Centre) kwa mfanyabiashara yeyote mwenye dhamira ya kuwekeza nchini. Alitaja msaada wanaotoa kupitia kituo hicho ni pamoja na msaada wa kupata vibali vya kazi na makazi, kupata ardhi ya kuwekeza, miongozo ya kodi ikiwemo kupata Namba ya Utambulisho ya Mlipa Kodi (TIN), kuthibitisha bidhaa kutoka Shirika la Viwango Tanzania, Mamlaka ya Chakula na Dawa na masuala ya kupata vibali vya mazingira (environment clearance).

Bw. Mnali alibainisha kuwa kuna bandari kubwa tatu nchini zinaunganisha nchi jirani ambazo hazina bandari. Aidha, Tanzania inaongoza kikanda kupokea miradi ya moja kwa moja ya uwekezaji kutoka nje (FDI) na pia ni miogoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi duniani. Alisema sababu hizo ni vigezo tosha vya kuichagua Tanzania kuwa kimbilio la uwekezaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Wafanyabiashara la Umoja wa Ulaya nchini, Bi. Marie Strain alisema kuwa nchi za umoja huo zinashika nafasi ya pili kwa kufanya biashara na Tanzania. Hivyo kundi hilo linatoa huduma mbalimbali kwa Wafanyabiashara zikiwemo za ushauri, taarifa za masoko na maeneo ya uwekezaji pamoja na kufanya majadiliano na Serikali namna ya kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji.

Katika mahojiano na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga alisema kuwa ujio wa wawekezaji hao unatokana na juhudi za Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji za kuvutia wawekezaji. Alisema Ubalozi umefanya hivyo, huku ukitambua kuwa takwimu zinaonesha kuwa Ubelgiji ni moja ya nchi kumi duniani zinazoongoza kwa kufanya uwekezaji nje ya nchi.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dar Es Salaam, Tanzania

25 Oktoba 2018

Tags: biasharaFDIkilimomiundombinuStella ManyanyaTICTINuwekezajiuzalishajiviwanda
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko.

Wahandisi wazalendo washauriwa kuchangamkia fursa

Discussion about this post

Habari Mpya

Serikali, Benki ya Dunia wajadili ushiriki Sekta binafsi

March 30, 2023
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Msiwabanie vijana wajasiriamali: Majaliwa

March 28, 2023
Lusaka-Zambia. Picha|Mtandao

Watanzania watakiwa kuchangamkia fursa Zambia

March 27, 2023
Waziri  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa, Adolf Mkenda.

Waziri wa Elimu azungumza na Benki ya Dunia

March 27, 2023

Bilioni 647.5 kuitoa Kagera gizani

March 17, 2023
Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba.

44.4bn kutumika matumizi ya kawaida na maendeleo

March 13, 2023

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Serikali, Benki ya Dunia wajadili ushiriki Sekta binafsi

by Pesatu Reporter
March 30, 2023
0

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru amesema Serikali inafanya majadiliano ya kimkakati na Benki ya Dunia...

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Msiwabanie vijana wajasiriamali: Majaliwa

by Pesatu Reporter
March 28, 2023
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza viongozi wa Mkoa wa Simiyu wasiwabane wajasiriamali, wawaelimishe na kuwapa miongozo ili wajiendeleze kiuchumi. Majaliwa...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In