Home BIASHARA Soko la pilipili lashuka

Soko la pilipili lashuka

0 comment 126 views

Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amesema soko la zao la pilipili hoho limeshuka katika miaka ya hivi karibuni tofauti na hali iliyokuwa miaka ya nyuma. Naibu Waziri huyo amesema hayo wakati akijibu swali la mwakilishi kutoka jimbo la Paje aliyetaka kufahamu sababu zilizopelekea zao hilo kupotea sokoni licha ya kwamba lilikuwa likifanya vizuri siku za nyuma.

Katika maelezo yake, Hafidh amedai kuwa serikali kupitia Shirika la Biashara Zanzibar (ZSTC) imekuwa ikichukua hatua stahiki kuhakikisha zao hilo linazalishwa kwa wingi  na kupata soko la uhakika. Vilevile Naibu huyo ameeleza kuwa serikali imekuwa ikihamasisha wakulima kulima mazao ya viungo kwa wingi na pilipili hoho imekuwa moja kati ya mazao hayo.

Mbali na hayo, Naibu Waziri Hafidh pia amesema wizara yake imekuwa ikiuza na kununua bidhaa za viungo za visiwani humo na kueleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018, ZSTC imetumia takribani Sh. 14,850,000 kununua bidhaa hizo ambazo ni pamoja na mdalasini, pilipili manga na pilipili hoho. Vilevile, shirika hilo limekuwa likisajili na kuhamasisha wa wakulima wa viungo ili kuchochea uzalishaji na kupata mazao yenye kukidhi haja.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter