Home BENKI Wanahisa Azania mambo shwari

Wanahisa Azania mambo shwari

0 comment 55 views

Wanahisa kutoka Benki ya Azania wameelezwa kufurahia ufanisi, mwenendo na mafanikio ya benki hiyo japokuwa sekta ya benki hapa nchini ilikumbwa na mtikisiko. Wanahisa hao wamedai kuridhishwa zaidi na jinsi benki hiyo ilivyofanikiwa kukabiliana na changamoto ya mikopo isiyolipika. Wakitoa maoni yao kwenye mkutano mkuu wa benki hiyo jijini Dar es salaam, wanahisa hao wamesema benki ya Azania imepiga hatua katika sekta kadhaa zikiwemo kukidhi matakwa ya Sheria za kibenki, ongezeko la rasilimali pamoja na kufanikiwa kukwepa changamoto ya mikopo isiyolipika.

“Kwa mujibu wa ripoti hii, ongezeko la rasilimali ni asilimia 15 na zaidi kinachovutia ni kuona kwamba benki yetu imejitahidi sana kukabiliana na tatizo la mikopo isiyolipika kwa kuwa asilimia nane tu ya mikopo, na wito wangu kwa uongozi wa benki ya Azania ni kuhakikisha asilimia hizi zinashuka hadi kufikia chini ya asilimia 6”. Amesema mwanahisa mmoja.

Katika taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Charles Itembe, imeelezwa kuwa ufanisi wa Azania umeonekana zaidi mwaka huu baada ya kutoa gawio la Sh. 633 milioni kwa wanahisa, ikiwa ni mara ya kwanza tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1995. Aidha, mafanikio katika utendaji yamewezesha benki hiyo kupata faida baada ya kodi ya Sh. 1.81 bilioni.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Makamu Mwenyekiti Eliudi Sanga amesema mafanikio ya benki hiyo kwa kiasi kikubwa yametokana na mabadiliko yaliyofanywa mwaka 2017 ambapo masuala mbalimbali yalibadilishwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter