Home BIASHARA TRA yawabana wafanyabiashara mitandaoni

TRA yawabana wafanyabiashara mitandaoni

0 comments 188 views

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imewata wafanyabiashara wa mitandaoni kuanza kulipa kodi kama ilivyo kwa wafanyabiashara wenye maduka ya kawaida nchini.

Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi Richard Kayombo wakati akiongea na pesatu.com ambapo alisema wajibu wa kwanza kwa mfanyabiashara yeyote ni kulipa kodi,hivyo wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali mitandaoni hupata wateja kama walivyo wafanyabishara wengine na wanatakiwa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria.

“Hizo ni biashara za kawaida kama nyingine isipokua zinafanyika kwa njia ya mtandao tu”

Pia kayombo alisisitiza umuhimu wa kulipa kodi kwa wafanyabiashara hao akiwafananisha na wale wa uber (magari ya kubebea abiria kwa njia ya mtandao) ambao wanalipa kodi japo ni biashara inayofanyika mtandaoni.

Kuhusu kuwadhibiti wafanyabiashara hao,kayombo aliwaomba walipe kodi kwa ridhaa yao kabla ya kufuatwa na sheria kuchukua mkondo wake.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!