Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amefanya ziara ya kutembelea na kukagua ufanisi wa utendaji wa bandari ya Dar es salaam ambapo ameonyesha kuridhishwa na maboresho makubwa yaliyofanywa jambo lililowezesha kuongezeka kwa kasi ya utoaji mizigo.
Katika ziara hiyo, RC Makalla amewahakikishia wananchi na wafanyabiashara ndani na nje ya nchi kuwa kazi katika bandari hiyo zinakwenda vizuri kufuatia mwekezaji wa kampuni ya TICTS kukabidhi jukumu la utoaji mizigo kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Aidha RC Makalla amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya upanuzi na ununuzi wa vifaa vya kisasa ili kuongeza ufanisi ambapo zaidi ya shilingi bilioni 200 zimetumika.
Kutokana na bandari hiyo kuwa tumaini na kimbilio la wengi, RC Makalla ameelekeza TPA kufanya kazi kwa weledi Ili kuonyesha uamuzi ya kukabidhi jukumu la utoaji mizigo haukukosewa.