Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itaiwekea thamani madini ya Tanzanite ili yapate bei kubwa sokoni.
Katika mwendelezo wa kurekodi Filamu itakayoonesha mazuri yaliyopo Tanzania, Rais Samia ameeleza kuwa “tumekwenda Mirerani (kunakochimbwa madini ya Tanzanite) kuonesha ulimwengu kuwa Tanzanite ni ya Tanzania, na tumekwenda kwenye machimbo na kuchukua picha inavyochimbwa, inavyopimwa inavyoongezwa thamani mpaka tunapata vito.
“Sasa wale wanaouza hovyo hovyo huko wajue kwamba iyo kitu kwao ni Tanzania. Na ulimwengu utaamini hivyo kwa sababu tunawaonesha. Kubwa zaidi tunataka kuiweka thamani Tanzanite yetu isizagae duniani hovyo hovyo itoke Tanzania kwenda sokoni ili tupate bei kubwa.” amesema.
Rais Samia anaendelea na ziara ya kurekodi filamu ya kuonyesha vivutuio mbalimbali vya utalii vilivyopo Tanzania katika maeneo mbalimbali. Filamu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa nchini Marekani.