Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amesema licha ya mlipuko wa Covid-19 ulioathiri uchumi wa nchi nyingi duniani, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zilizokuwa na ukuaji chanya wa uchumi kwa mwaka 2020.
Waziri Nchemba amesema pato la Taifa lilikuwa kwa asilimia 4.8 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 mwaka 2019.
Ukuaji huo chanya ulitokana na hatua ya serikali kuruhusu shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea.
Nchemba amesema hayo wakati akisoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2021/2022
Amezitaja sekta zilizokuwa kwa viwango vya juu kwa mawaka 2020 ni pamoja na sekta ya Ujenzi 9.1%, Habari na Mawasiliano 8.4, Uchukuzi na uhifadhi wa Mizigo 8.4%, Huduma zinazohusiana na Utawala 7.8%, Shughuli za Kitaalamu, Sayansi na Ufundi 7.3%, Madini na Mawe 6.7% na Afya na Huduma za Jamii 6.5%