Home BIASHARAUWEKEZAJI Mapato ya dhahabu yapaa Geita

Mapato ya dhahabu yapaa Geita

0 comment 110 views

Sheria mpya ya udhibiti wa mapato yatokanayo na madini hasa dhahabu yamesababisha kuongezeka kwa pato la serikali mkoani geita.

Mapato hayo yanadaiwa kupanda kwa zaidi ya mara mbili kutoka shilingi bilioni 56.2 kwa mwaka wa fedha 2017/18 hadi kufikia bilioni 114.7 kwa mwaka wa fedha 2017/18 na hivyo kuvuka lengo la ukusanyaji ambalo lilikua shilingi bilioni 51.

Kupanda huko kwa mapato inadaiwa ni matokeo ya mabadiliko ya sheria na ushirikishwaji wa vyombo vya dola ili kuhakikisha rasilimali hiyo ipo salama pamoja na kuongezeka kwa bei katika soko la dunia.

Wakati wa uzinduzi wa shughuli za uchenjuaji dhahabu utakaokuwa ukifanywa na kampuni ya jema African tawi la geita,baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa wamesema wanatarajia kuendelea kuongezeka kwa pato hilo kufuatia agizo la serikali la kuzuia usafirishaji wa cabon yenye dhahabu nje ya mkoa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter