Home BIASHARA Wafanyabiashara Afrika Mashariki kukutana Mwanza

Wafanyabiashara Afrika Mashariki kukutana Mwanza

0 comment 56 views

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na Chemba ya Biashara (TCCIA) mkoa wa Mwanza wanaandaa maonyesho ya 13 ya wafanyabiashara wa Afrika Mashariki yatakayofanyika Agosti 31 mwaka huu. Mkurugenzi wa Tantrade Edwin Rutageruka amesema maonyesho hayo yanalenga kuinua sekta ya viwanda na biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuzitangaza fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara.

“Naomba wafanyabiashara wayatumie maonyesho hayo kutafuta masoko endelevu na kutengeneza mitandao ya biashara Afrika Mashariki” Amesema Rutageruka.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TCCIA Mwanza Dk. Elibariki Mmari amewashauri wananchi kujenga utamaduni wa kujifunza masuala ya biashara kutoka nchi nyingine za Afrika Mashariki ambazo zinatarajia kushiriki maonyesho hayo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amesema serikali ya mkoa huo itahakikisha usalama wa kutosha kwa washiriki watakaojitokeza kuutangaza mkoa huo ili kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter