Home BIASHARAUWEKEZAJI Kigwangalla apigia debe uwekezaji sekta ya utalii

Kigwangalla apigia debe uwekezaji sekta ya utalii

0 comment 142 views

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla amewataka wawekezaji kufika nchini na kuwekeza katika sekta ya utalii. Kigwangalla amesema hayo katika kongamano la kumi la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya utalii Afrika nchini Hispania na kuwahakikishia wawekezaji kuwa, Tanzania mbali na Tanzania kuwa sehemu salama, pia kuna vivutio na fursa mbalimbali za kuwekeza.

Kongamano hilo lililofanyika jijini Madrid nchini Hispania limeandaliwa na Shirika la Utalii  la Umoja wa Mataifa (UNWTO)kwa kushirikiana na Taasisi za Casa Afrika pamoja na Taasisi ya maonyesho ya biashara ya Madrid (IFEMA) na kushirikisha nchi mbalimbali duniani.

“Nawakaribisheni nyote, Njooni Tanzania muwekeze kufuatia uwepo wa mazingira na miundombinu bora kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya utalii pamoja na viwanda”. Amesema Waziri huyo.

Aidha, Waziri Kigwangalla ametaja baadhi ya jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kuwa ni pamoja na kufufua Shirika la Ndege la ATCL, kujenga chanzo kikubwa cha kuzalisha  umeme katika mto Rufiji, mradi wa kisasa wa ujenzi wa njia mpya ya kisasa ya reli (Standard Gauge) pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter