Home BIASHARAUWEKEZAJI Mkutano wa Korea kufungua milango ya uchumi, teknolojia Afrika: Samia

Mkutano wa Korea kufungua milango ya uchumi, teknolojia Afrika: Samia

0 comment 273 views

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ana imani mkutano wa Korea na Afrika utafungua milango ya ushirikiano wa kiuchumi na teknolojia kwa faida ya maendeleo ya Afrika.

Rais Samia ameeleza hayo katika mkutano wa Korea na Afrika unaofanyika Jamhuri ya Korea kwa lengo la kujenga ushirikiano baina ya nchi hiyo na bara la Afrika.

Pia Rais Samia amesema kuna fursa ya kipekee katika kuunda ushirikiano wenye malengo mahsusi ya kiuchumi ili kutafuta ufumbuzi wa tofauti za maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi za Afrika.

“Rais Samia, anatarajia nia thabiti ya Korea katika mafanikio ya pamoja na kuunga mkono kuundwa kwa mpango kazi wa kushirikiana kwenye biashara na uwekezaji bila kusahau sekta binafsi,” imesema taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus.

Pamoja na kampuni moja ya Korea kushirikiana na Tanzania kwenye madini ya kinywe, Rais Samia amewakaribisha wengine nchini kwa ajili ya ushirikiano zaidi kwenye uchimbaji na utafiti wa madini ya kimkakati.

“Rais kama kinara wa masuala ya nishati safi barani Afrika ambayo itawasaidia sana wanawake amesisitiza umuhimu wa kuwekeza kwenye nishati hiyo sit u kwa ajili ya kupunguza hewa chafu, ila pia kupunguza uharibifu wa mazingira,” inaeleza taarifa ya Ikulu.

Wakati huo huo, Rais Samia alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Korea (KOICA) Chang Won Sam ambapo wamezungumzia namna ya kuendeleza ushirikiano wa miradi mbalimbali.

KOICA hadi sasa inatekeleza miradi 10 katika sekta za maji, afya na elimu ikiwemo kuimarisha afya ya mama na mtoto, kuanzisha huduma za usambazaji maji kw maeneo ya mjini na vijijini ikiwemo Dodoma na Arusha.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter