Home BIASHARAUWEKEZAJI Nyongo aagiza wamiliki wa mgodi kukamatwa

Nyongo aagiza wamiliki wa mgodi kukamatwa

0 comment 171 views

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameagiza kukamatwa kwa wamiliki wa mgodi wa Nyakavangala unaomilikiwa na Thomas Masuka kwa ushirikiano na wawekezaji wengine wazawa wapatao 20 kufuatia wamiliki hao kutofautiana kuhusu taarifa waliyoiwasilisha kwa Naibu Waziri juu ya namna ambavyo mgodi huo unaendeshwa ikiwemo masuala ya ulipaji kodi na mrabaha wa serikali.

Nyongo amewataka wamiliki hao kutoa maelezo yaliyojitosheleza kuhusu lini watakamilisha malipo ya kodi zote wanazodaiwa na serikali. Mgodi huo unadaiwa zaidi ya Sh. 128 milioni za mrabaha.

Akiwa ziarani mkoani Iringa, Naibu Waziri alisema kuwa pamoja na kuona shughuli za uchimbaji katika migodi ya dhahabu ya Ulata na Nyakavangala, pia amegundua ukwepaji mkubwa wa kodi na mrabaha wa serikali.

“Hatutaki ugomvi hapa kwenye migodi. Tunataka mgodi ufanye kazi. Dhahabu ziuzwe mahali panapoonekana. Hapa naona hesabu za viroba tu. Mnunuzi wa dhahabu hapa ni nani?” Amehoji Naibu Waziri.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amewataka wamiliki hao kujadili na kukubaliana namna ya kulipa fedha hizo huku akimuagiza Afisa anayehusika na masuala ya kusimamia fedha kutoka Halmashauri kuhakikisha fedha zote  ambazo mgodi huo ulitakiwa kulipa kama mrabaha zinapatikana.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter