Home BIASHARAUWEKEZAJI Rais Samia aahidi kufanya “Royal Tour” kuitangaza hifadhi ya Katavi

Rais Samia aahidi kufanya “Royal Tour” kuitangaza hifadhi ya Katavi

0 comment 91 views

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kufanya filamu nyingine ya Royal Tour katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi baada ya kujionea wanyamapori mbalimbali katika Hifadhi hiyo.

Dkt. Samia ameyasema hayo Julai 15, 2024 wakati akizungumza na wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Mkoani Katavi.

Kauli hiyo inafuatia ombi la Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, la kuomba Royal Tour nyingine ifanyike mkoani humo.

Hifadhi ya Katavi

“Nataka nikiri kwamba zile sifa alizozisema Waziri Mkuu Mstaafu kuhusu uwepo wa wanyama wengi na wa kuvutia katika Hifadhi ya Katavi nimeziona mwenyewe na zimetimia maana leo nilipita kwenye mbuga hiyo kuona ikoje mahitaji yakoje” amesema Rais Samia na kusisitiza:

“Tumeona mambo mengi ya kufanya mle ndani na suala la Royal Tour Waziri wa Maliasili na Utalii ameshaandika hivyo jipange na ukiwa tayari mimi mwenyewe nitakuja.

Soma: Royal Tour yaongeza mapato kutoka Tsh 70bn hadi Tsh 84bn

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter