Home KILIMO Waliolipwa korosho kuwekwa hadharani

Waliolipwa korosho kuwekwa hadharani

0 comment 61 views

Ili kuondoa sintofahamu katika jamii, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ameagiza wataalamu wa timu ya Oparesheni Korosho kubandika majina ya wakulima wote ambao tayari wamelipwa na serikali. Hasunga amesema hayo mkoani Mtwara alipokuwa akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mifugo na Maji. Waziri huyo amedai mkakati huo unalenga kupunguza lawama kutoka kwa wakulima ambao hawana nia njema na serikali.

“Mimi nashangaa sana kila mkulima akiulizwa anasema hajalipwa jambo hili sio sawa nadhani wanafanya hivi kukwepa madeni wanayodaiana huko vijijini, sasa naitaka timu ya wataalamu wa Oparesheni Korosho kuhakikisha majina yote ya wakulima waliolipwa yanabandikwa kwenye ofisi za vijiji. Mpaka sasa tani 222,684 zimekwisha kusanywa huku hadi kufikia tarehe 14 Machi 2019 tayari jumla ya Sh. Bilioni 596.9 zilikuwa zimekwishalipwa kwa wakulima kati ya Sh. Bilioni 723 lakini nashangaa wakulima wanasema hawajalipwa hili sio sawa”. Amesema Waziri huyo.

Pamoja na hayo, Waziri Hasunga amesisitiza kuwa hadi kufikia mwisho wa mwezi huu, wakulima wote watakuwa wamelipwa fedha zao kwani uhakiki umekamilika kwa kiasi kikubwa. Hasunga amesema serikali inatakiwa kuungwa mkono kwa uamuzi wake wa kuwalipa wakulima Sh. 3,300 kwa kila kilo moja ya korosho.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter