Home BIASHARAUWEKEZAJI Uagizaji wa luku nje kufikia tamati Julai

Uagizaji wa luku nje kufikia tamati Julai

0 comment 89 views

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani ametangaza kuwa ifikapo mwezi Julai mwaka huu, serikali itasitisha rasmi uagizaji wa mita za luku ya umeme kutoka nje ya nchi ili kuinua wawekezaji wa ndani. Dk. Kalemani amesema hayo wakati akizindua kiwanda cha kutengeneza luku cha Baobab Energy System Tanzania (BEST) jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa, uwekezaji huo utaokoa gharama za usafirishaji kutoka nje ya nchi.

Waziri huyo amedai kuwa kusitisha zoezi hilo ni muendelezo wa mkakati wa serikali ya awamu ya tano kutoa fursa zaidi kwa wawekezaji wa ndani. Amesema kuwa hapo awali, serikali ilisitisha uagizaji wa nguzo kutoka Afrika Kusini na transfoma kutoka nchini India kwani serikali ilikuwa ikitumia gharama kubwa kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kiwanda hicho Hashimu Ibrahimu amesema kiwanda hicho kimeanzishwa kwa lengo la kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli katika jitihada zake za kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda ifikapo 2025.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter