Home KILIMO Majaliwa mgeni rasmi kongamano la wakulima

Majaliwa mgeni rasmi kongamano la wakulima

0 comment 62 views

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la siku tatu la wakulima wapatao 2,400 kutoka maeneo mbalimbali nchini. Kongamano hilo  litakalofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro Oktoba 3 linaadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata).

Akizungumza na waandishi, Mkurugenzi Mtendaji wa Mviwata, Stephen Ruvuga amesema Waziri Mkuu atafungua maadhimisho hayo na atapata nafasi ya kufanya mazungumzo na wakulima hao. Ruvuga ameongeza kuwa, kongamano hilo litaambatana na  kongamano la kitaifa la wakulima kuhusu ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Akielezea kuhusu kongamano hilo, Ruvuga amesema kutakuwa na majadiliano kuhusu jinsi gani wakulima wanaweza kujipanga na kuwa washiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda pamoja na kuangalia nyenzo muhimu za kufanikisha ushiriki wa wakulima wadogo katika mfumo wa uchumi wa viwanda ikiwa ni mkakati wa serikali ya awamu ya tano

Watu mbalimbali wanatarajia kushiriki katika kongamano hilo wakiwemo mawaziri, wabunge, viongozi na watendaji waandamizi, Kamishna wa ardhi, wawakilishi wa balozi, Prof. Issa Shivji, washirika wenza, marafiki wa Mviwata na wadau wengine wa kilimo kutoka ndani na nje ya nchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter