Kufuatia mkutano wa Baker McKenzie unaofanyika huko Johannesburg mwezi huu, wanasheria wa Baker McKenzie kwa Afrika, wataalamu wa kimataifa wa kampuni hiyo kwa Afrika na wanasheria kutoka makampuni ya uhusiano wa kiafrika kutoka barani kote, kwa pamoja wamebadilishana ujuzi kuhusu mambo ambayo wawekezaji wanatakiwa kuzingatia wakati wanataka kuhusiana na Afrika katika masuala ya uwekezaji.
Wameyataja mambo hayo kuwa ni:
Kukubaliana na mambo wasiyoyajua na kukusanya ujuzi
Wawekezaji Afrika wanapaswa kuzingatia hali ya kisiasa na kiuchumi katika bara na pia utawala maalum wa nchi na kanda, utekelezaji na changamoto za udhibiti wakati wa kuwekeza katika kanda. Pia wanapaswa kukabiliana na ukosefu mkubwa wa miundombinu na ushirikiano wakati wanashughulika katika mipaka ya Afrika. Ili kufungwa mikataba barani Afrika, wawekezaji wanahitaji kupata habari na nyaraka sahihi. Mafanikio katika shughuli nzima yanategemea na ujuzi halisi na si mtizamo wa soko kwa muda huo. Kuhusu masoko kuwa na habari za kuaminika, washirika wa kuaminika kimataifa, kikanda na hata kwa wenyeji ni muhimu. Kwa sababu kikawaida wawekezaji hawajali changamoto, lakini huwa hawajui jinsi ya kushiriki katika mambo wasiyoyajua.
Hakuna njia moja ya kuwekeza Afrika
Wawekezaji hawatakiwi kufikiri kwamba nchi moja ni sawa na nchi nyingine barani Afrika. Hata kama zina ujirani kijiografia, ifahamike kuwa kila nchi ni tofauti na nyingine. Mfumo wa kisheria katika nchi nyingi pia unabadilika haraka, unaosababishwa na hamu ya kuhamasisha uwekezaji wa kigeni, lakini pia unabadilika ili kulinda haki na rasilima;I za nchi na watu wake.
Wawekezaji wanapaswa kujadili miongoni mwa sheria na kanuni katika mazingira yenye changamoto. Matokeo yake, kufuata kisheria katika mpakani imekuwa ngumu sana kwa sababu wawekezaji wanasema ni moja ya hatari kubwa kibiashara kwa Afrika.
Rushwa, Utawala, Sera
Hatua ya kufanya mambo kinyume na sheria, na utawala ikiwa ni pamoja na rushwa ni baadhi ya mambo ambayo yamewaongezea tahadhari wawekezaji barani Afrika. Sheria kali za kupinga rushwa katika baadhi ya nchi za wawekezaji, kama vile Marekani na Uingereza, zimefanya wawekezaji wa kigeni kuwa na wasiwasi. Wawekezaji wanatakiwa kufuata sheria na kanuni ili kuepuka kujihusisha na tabia zisizofaa na kuhakikisha wanaweza kufunga mikataba kwa haraka na kwa mafanikio.
Nchi kama Ghana na Rwanda (ukiachana na changamoto za hapa na pale) wanajitahidi kuweka usawa kwa kuwahamasisha wawekezaji na haki za nchi na watu wake. Katika nchi hizi hakuna wasiwasi mkubwa katika swala la utawala na zinavutia maslahi mengi ya wawekezaji. Pia nchi kama Botswana ingawa ni nchi ndogo lakini wawekezaji wanataka kuijua zaidi. Nchi hizi zimewapa wawekezaji uhakika na uwazi na sasa wanavuna faida za utawala wao mzuri.
Baadhi ya nchi ambazo zina uwezo wa kuwavutia wawekezaji lakini wanahitaji kufanya juhudi zaidi ni pamoja na Kenya, Afrika Kusini na Nigeria kwa sababu wapo vizuri katika mambo mengine lakini kuna wasiwasi katika utawala na uwezo wao wa kutekeleza sera nzuri kwa wawekezaji. Hivyo nchi hizi zinatakiwa kuzingatia kuongezeka kwa uhakika na uwazi kwa wawekezaji na kuhakikisha kuwa sera mpya zilizotengenezwa zinaenda kimpangilio na ni thabiti.
Tahadhari kwa vichwa vya biashara kimataifa na kikanda
Kuongezeka kwa hatari ya kuwekeza Afrika ni pamoja na mvutano wa kimataifa ambao umekuwa ukiendelea baina ya China na Marekani kuhusu asilimia 25 ya ushuru ambazo Marekani imeweka katika bidhaa zinazoagizwa kutoka China. Ifahamike kuwa, China inafanya biashara sana na Afrika, hivyo mvutano baina ya mataifa hayo unaweza kuathiri Afrika. Pia suala la kutokuwepo na mpango wa Brexit (no deal Brexit) kunaweza kuongeza vikwazo vya biashara na kuharibu uwekezaji wa biashara ikiwa ni pamoja na barani Afrika.
Uwekezaji katika miundombinu na maendeleo ya uchumi wa kikanda
Ili kuongeza uwekezaji na kuwezesha uchumi wa Afrika ikiwa ni pamoja na kutumia fursa zilizopo swala la kuendeleza miundombinu ni muhimu. Hivyo miundombinu inatakiwa kuendelezwa ili kuunganisha nchi za barani Afrika. Hii itaongeza urahisi wa shughuli za mipaka na kukua uwekezaji katika kanda za Afrika kwa ujumla.
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), imeeleza kuwa miundombinu duni imepunguza ukuaji wa Afrika kwa asilimia 25 katika miaka miwili iliyopita. Pia Benki ya Dunia (WB) inakadiria kuwa bara inahitaji zaidi ya dola bilioni 90 kwa mwaka ili kuanza kuziba pengo la miundombinu.
Ripoti ya Baker McKenzie na IJGlobal, ‘A changing world’ inaeleza kuwa muelekeo mpya katika utoaji wa fedha za miundombinu ya soko unaonyesha kuwa mikopo ya maendeleo ya maendeleo ndiyo sababu muhimu zaidi katika ufadhili wa miradi ya miundombinu ya Afrika.
Vilevile, ripoti hiyo ilibainisha kuwa China inaweka dola bilioni 8.7 katika miradi ya miundombinu Afrika ya kusini katika jangwa la Sahara kwa mwaka 2017 peke yake, wakati Marekani hivi karibuni imeanzisha shirika jipya la US $ 60,000,000 kuwekeza katika nchi zinazoendelea.
Muda unaua mikataba
Ukosefu wa kasi ya utekelezaji wa mradi unaweza kuua shughuli nzima. Kushughulika na sera za serikali zenye nguvu na mifumo tata ya kisheria zinaweza kuongeza muda mwingi wa kushughulikia, na hata kuchelewesha. Ili kuepuka hilo ni muhimu kwa wawekezaji kushirikiana na washauri wenye ujuzi katika mambo ya sera, mifumo ya kisheria na uelewa kuhusu maeneo ya uwekezaji.
Wawekezaji pia wanategemea washauri wao kutumia tekinolojia za kisasa katika upande wa sheria (legaltech) ili kuhakikisha ufanisi na ufungaji wa mikataba unafanyika kwa kasi. Afrika imeendelea katika teknolojia kwa namna moja au nyingine lakini teknolojia katika masuala ya sheria bado iko nyuma.
Wakati makampuni mengi madogo ya sheria yanatafuta gharama za utekelezaji wa lawtech kuwa marufuku, suluhisho liko katika kushirikiana na makampuni makubwa duniani ambayo yanaweza kushiriki upatikanaji wa teknolojia yao. Kwa miaka mingi Baker McKenzie amejulikana kwa mbinu yake ya kufikiria mbele kuhusu uvumbuzi. Kampuni hiyo imebuni mfumo wa utoaji wa huduma zake za kisheria kwa ubunifu, kwa kuuliza wateja wake nini wanahitaji na kisha kujenga suluhisho pamoja na wateja.
Washirika sahihi wa biashara Afrika
Ili kutumia fursa hali ya hewa nzuri kwenye uwekezaji, wawekezaji wanapaswa kuunda uhusiano wa karibu na mshauri bora wa kisheria, pamoja na wataalamu wenye bidii na washauri wa ndani barani Afrika ambao wana ujuzi wa kitaaluma na uelewa wa changamoto fulani za biashara ndani ya maeneo yao ya uwekezaji