Home BIASHARAUWEKEZAJI Waziri Mkuu atembelea Kituo cha Uwekezaji

Waziri Mkuu atembelea Kituo cha Uwekezaji

0 comment 92 views

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameagiza Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kumaliza urasimu ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake na kuongeza kuwa, eneo hilo linahitaji umakini wa hali ya juu hivyo ni muhimu kwa TIC kuhakikisha kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maslahi ya taifa. Majaliwa amesema hayo alipozungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa TIC pamoja na Menejimenti jijini Dar es Salaam ambapo ameagiza uongozi wa kituo hicho kuweka kipaumbele cha kwanza katika kulinda rasilimali za nchi na maliasili zake ikiwemo ardhi, mazao ya uvuvi, misitu, madini.

“Katika kuvutia wawekezaji hasa wa nje ni lazima tuweke kipaumbele katika kulinda rasilimali zetu kama ardhi, madini, fukwe ili zisiporwe kwa kisingizio cha uwekezaji.” Ameeleza Waziri Mkuu.

Aidha, Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa kituo hicho kuhakikisha kinatekeleza majukumu yake n kueleza kuwa ili kupata matokeo mazuri, ni lazima kituo hicho kuimarisha mawasiliano na uratibu miongoni mwa wadau wote na kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa.

“Serikali imedhamiria kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025, TIC inatakiwa iongoze kwa kuvutia wawekezaji wengi wa ndani na nje ya nchi”. Amesisitiza Majaliwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter