Home VIWANDANISHATI Kisima cha gesi hatarini kumezwa na bahari Mtwara

Kisima cha gesi hatarini kumezwa na bahari Mtwara

0 comment 33 views

Naibu Mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji gesi ya Maurel & Prom Tanzania Elias Kilembe amemueleza Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani kuwa, huenda nchi ikajikuta gizani endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kufuatia kina cha bahari ya Hindi katika eneo la Mnazi Bay Msimbati mkoani Mtwara kuendelea kumomonyoka kila siku kuelekea nchi kavu. Naibu Mkurugenzi huyo amesema hayo wakati Dk. Kalemani alipotembelea visima hivyo vya  gesi.

Kilembe ameeza kuwa siku hadi siku, bahari imeendelea kusogea nchi kavu kuelekea mahali kilipo moja ya kisima cha gesi na mitambo, hali ambayo amesema inawapa wasiwasi.

“Hata mwaka jana ulitokea mmomonyoko lakini haukuwa tishio kama wa mwaka 2015, lakini ukija hapa baharini unakuta mchanga umeondoka wote na kupotea, kweli ni tishio kwa kambi hii”. Amesema Kilembe.

Baada ya kujionea hali halisi, Dk. Kalemani ameshauri kujengwa kwa ukuta mara moja ili kutenganisha kisima  kilipo na bahari, lengo likiwa ni kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

“Kuanzia sasa anzeni kufanya utaratibu wa kujenga ukuta kwa sababu mtafika mahala mtakosa hata pa kuweka ukuta maji yakishafika huku, ni vizuri kuanza sasa ili msije kukumbwa na dhoruba kubwa, haya ni maagizo ya haraka haraka wala si jambo la kufanya utafiti”. Amesema Dk Kalemani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter