Home BIASHARA Vodacom yazindua mnara wa kwanza wa simu Wilayani Longido

Vodacom yazindua mnara wa kwanza wa simu Wilayani Longido

0 comment 146 views

Vodacom Tanzania imezindua mnara wa kwanza wa simu za mkononi wilayani Longido kata ya Mundarara eneo mahususi linalofanyika shuhuli za uchimbaji wa madini ya Ruby Mkoani Manyara.

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mh Frank Mwaisumbe (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Kanda ya Kazikazini wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bi Brigita Stephen (kushoto) wakipewa maelezo na Mkandarasi wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bw. Isaac Peter Olesingo juu ya uwezeshaji wa mawasiliano utakaosaidia shuhuli za kiuchumi kijijini hapo ambapo shuhuli za uchimbaji wa madini ya Ruby zinafanyika.

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mh Frank Mwaisumbe akizungumza na wachimbaji wa madini ya Ruby na wanakijiji wa Kata ya Mundarara Wilaya ya Longido juu urahisi wa mawasilioano haswa kwa wafanya biashara wa madini ya Ruby baada ya uzinduzi wa mnara wa kwanza wa simu kijijini hapo uliozinduliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Bw Frank Mwaisumbe (kulia), Mkurugenzi wa Kanda ya Kazikazini wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bi Brigita Stephen (kati) na Diwani wa Kata ya Mundarara, Bw Alais Mshao (kushoto) wakipewa maelezo na Mkandarasi wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bw. Isaac Peter Olesingo juu manufaa ya kiuchumi yatakayo tokana na mnara huu wa kwanza wa simu kufikisha mawasiliano kijijini hapo ambapo shuhuli za uchimbaji wa madini ya Ruby zinafanyika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter