Home BIASHARA Wafanyabiashara wachekelea agizo la JPM

Wafanyabiashara wachekelea agizo la JPM

0 comment 98 views

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Stephen Chamle amesema jumuiya hiyo imefurahishwa na agizo la Rais Magufuli kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo mamlaka hiyo imetakiwa kuangalia upya viwango vya ulipaji wa kodi ili kuepusha mazingira yoyote ya ukwepaji kodi. Chamle amesema mapitio hayo yakifanyika, itakuwa rahisi kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ambao wamekuwa waathirika wakubwa wa tozo hizo.

“Hii itasaidia kuvutia biashara kubwa Tanzania na tunapendekeza maeneo yatakayofaa ikiwamo Kariakoo, Mwanza, Tanga, Songwe, Mtwara, Dodoma pamoja Kigoma”. Amesema

Pia amesema kuwa kama serikali itaweka kodi elekezi sehemu kama Forodha, itasaidia wafanyabiashara kuacha kukwepa kodi na vilevile rushwa itapungua. Aidha wameshauri serikali kuelekeza kodi ya Ongezeko la thamani ‘VAT’ viwandani, mipakani, bandarini, katika viwanja vya ndege na wasambazaji wakubwa na kuiondoa madukani.

“Ili kuziba pengo dogo litakalojitokeza, kiwango cha VAT kutoka asilimia 18 hadi 21 na kuondoa msururu wa kodi, udanganyifu wa nyaraka na kuliacha soko kuwa huru na itachochea ustawi wa biashara nchini”. Amesema Mkurugenzi huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter