Home BIASHARA Wafanyabiashara wanaokwepa kodi kubanwa

Wafanyabiashara wanaokwepa kodi kubanwa

0 comment 116 views

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji ametoa siku moja kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukabidhi taarifa ya idadi ya mashine mbovu za kielektroniki maarufu kama EFD zilizopo Kariakoo jijini Dar es salaam, ili serikali iweze kubaini wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa makusudi. Dk. Kijaji amesema hayo baada ya kupita na kununua vitu mbalimbali katika eneo hilo ambapo baadhi ya maduka walidai mashine zao ni mbovu hivyo kushindwa kumpatia risiti za EFD.

“Kama Wizara tunahitaji kupata haya yote kuhusu udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara wa Kariakoo, ikiwa ni pamoja na kujua kuna mashine ngapi mbovu. Hiki kipindi watu wengi wananunua hivyo wafanyabiashara wasipotumia mashine tunapoteza kodi nyingi. Tunataka kujua tumepoteza kodi kiasi gani tangu mwezi Septemba mwaka huu hadi sasa katika duka hili la vifaa vya michezo kwa kuwa mashine yao imekuwa mbovu kipindi chote hicho. Hiki ndicho kimenizuia nisiende Dodoma ili nishughulike na suala hili kwanza”. Ameeleza Dk. Kijaji.

Aidha, Dk. Kijaji amesisitiza kuwa, hakuna taifa linalopata maendeleo pasipo wananchi kulipa kodi na kuwataka wafanyabiashara kufika ofisi husuka wanapokutana na tatizo. Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa kodi za ndani kutoka TRA, Abdul Mapembe amesema wamepokea maagizo hayo na tayari wameanza kuyafanyia kazi huku akisisitiza kuwa, zoezi la kuwasaka wafanyabiashara wanaokwepa kodi ni endelevu kwani baadhi yao wamekuwa wakifanya vitendo hivyo kwa makusudi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter