Home BIASHARA Wanawake kupewa kipaumbele uwekezaji

Wanawake kupewa kipaumbele uwekezaji

0 comment 113 views

Katika kuinua wanawake katika sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu ameahidi kuanzisha dirisha maalumu litakalo wasaidia wanawake katika uwekezaji ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanapotaka kuwekeza.

Waziri Ummy amesema atahakikisha anatoa kipaumbele kwenye kutoa vibali vya Mazingira ili mradi tu biashara au uwekezaji unafanywa na mwanamke.

Ameyasema hayo katika hafla ya utoaji Tuzo za Viwanda kwa Wanawake Wajasiriamali Tanzania iliyoandaliwa na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

“Kupitia NEMC ninawaahidi kuanzisha dirisha maalum la biashara na uwekezaji ili kuweka mazingira mazuri kwa mwanamke anayetaka kuwekeza awekeze bila vikwazo, moja ya kipaumbele ni kuhusu vibali kutoka kwa wakati” amesema Waziri Ummy.

Amewata wanawake kutokata tamaa na kuondoa uwoga wanapotaka kufanya uwekezaji. Amesema”ndugu zetu wanaume hawaogopi ndiyo maana wapo mbali katika kufanya biashara na uwekezaji, nasisitiza kuwa mwanamke aondoe hofu anapotaka kuwekeza, afanye kazi kwa bidii ili aweze kufikia malengo na mafanikio makubwa”.

Aidha, ametoa rai kwa wanawake kuchangamkia fursa kwenye sekta ya mazingira, mfano kupitia marufuku ya mifuko ya plastiki watengeneze mifuko mbadala. Pia watumie nishati mbadala wakati wa uzalishaji kuliko kutumia nishati ya miti, hii itasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira na kuzuia mabadiliko ya tabia nchi.

Mkurugenzi wa Idara ya Watoto, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mwajuma Magwiza, amesema kupitia mamlaka za Serikali za Mitaa, Serikali imekuwa ikitenga fedha za mikopo yenye masharti nafuu kwa wanawake kupitia vikundi ili kuwapa fursa ya kuanzisha biashara na uwekezaji.

Rais wa wanawake wajasiriamali Tanzania, Maida Waziri, amesema adui wa mwanamke siyo mwanamke bali ni umasikini, wanawake washirikiane kuukataa umasikini kwa vitendo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter