Home Elimu Serikali ya Tanzania yatakiwa kujenga maabara za TEHAMA katika kila shule

Serikali ya Tanzania yatakiwa kujenga maabara za TEHAMA katika kila shule

0 comment 133 views

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Oran Njeza ameiagiza Ofisi ya Rais- TAMISEMI kuhakikisha inajenga maabara za TEHAMA katika kila shule ili wanafunzi wapate ujuzi kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani.

Ameyasema hayo Mei 21, 2024 kwenye kikao cha kujengewa uwezo wajumbe wa kamati hiyo kuhusu ufundishaji mubashara uliofanyika katika darasa janja katika Shule ya Sekondari Dodoma jijini Dodoma.

Njeza amesema TEHAMA ndiyo inayojenga dunia kwa sasa hivyo ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kila shule inayojengwa inakuwa na maabara za TEHAMA na kuhakikisha zinaongezeka kutoka maabara 3 hadi nne.

Ameitaka Serikali kuhakikisha kila shule inakuwa na maabara ya TEHAMA ili wanafunzi wakitoka shuleni wawe na elimu ya kutosha ya masuala ya TEHAMA na kuleta mabadiliko katika kujifunza na kufundishia

Aidha Kamati imeridhishwa na matumizi ya madarasa janja kwa ajili ya kujifunzia na kufundishia ambapo wameweza kuona matumizi ya TEHAMA yanavyoweza kufundisha shule ya Sekondari Dodoma, Dr Samia, Kibaha iliyopo Mkoa wa Pwani na shule ya sekondari ya Mtakuja ya Zanzibar.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Zainab Katimba ameieleza Kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa Serikali imepanua wigo wa matumizi ya TEHAMA katika kufundisha wanafunzi ili kupunguza changamoto ya upungufu wa walimu nchini.

Zipo njia nyingi za kukabiliana na changamoto ya walimu, njia hizo ni pamoja na kuendelea kuajiri walimu na kutumia TEHAMA katika kufundisha na kujifunza.

Vilevile ameileza kamati kuwa ni maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa kuhakikisha kila Halmashauri inatenga fedha za mapato ya ndani ya kuanza kujenga madarasa janja pamoja na ngazi ya Mikoa kujenga kituo kimoja cha TEHAMA katika ngazi ya Mkoa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter