Home FEDHABIMA Jamii yahamasishwa kujiunga na Bima ya Afya

Jamii yahamasishwa kujiunga na Bima ya Afya

0 comment 95 views
Na Mwandishi wetu

Taasisi ya Nordic Foundation Tanzania (NOFOTA) imezindua kampeni inayolenga kuhamasisha wananchi kujiunga kwa hiari na huduma ya bima ya afya kwa kupitia bahati nasibu ya ‘Afya Bando’ ambayo itatoa kadi za bima ya afya zaidi ya kumi kila wiki.

Ofisa Mipango Afya wa taasisi hiyo Maria Nimrod amesema wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa kampeni hiyo itakuwa ni mkombozi kwa watu wote katika jamii kwani ni falsafa ya ubinadamu na umoja katika bima ya afya.

Amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikijihusisha na masuala ya kijamii tangu ilipoanzishwa mwaka 2014 hivyo kampeni hiyo haitokuwa ya kibiashara. Afya Bando inalenga kuboresha afya ya rasilimali katika uchumi wa viwanda.

Naye Mtaalamu Mwelekezi wa kampeni hiyo Dk. Resipicius Salvatory amewataka wananchi kuondoa mawazo hasi kuhusiana na bima ya afya na kushauri wajitokeze kwa wingi kujiunga.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter