Home FEDHABIMA Umuhimu wa bima kwa wafanyabiashara

Umuhimu wa bima kwa wafanyabiashara

0 comment 149 views

Mara baada ya kuanzisha biashara, jambo la muhimu ni kujua namna ya kuilinda biashara yako isiharibike, kufa au kupotea. Kuilinda kwa maana ya dhidi ya wezi, majanga ya asili kama tetemeko na yale yasababishwayo na mwanadamu kama moto. Ipo njia moja na pekee inayoweza kusaidia katika kuilinda biashara yako au mali yako ambayo ni bima.

Bima ni mabadilishano kama fidia kati ya mmiliki wa biashara na kampuni ya bima katika kiwango fulani na kwa muhula/kipindi maalum. Kulipia bima kwa biashara yako ni kuikinga biashara yako isipate hasara endapo tatizo lolote lisilotarajiwa kama vile moto, wizi au majanga ya asili yatatokea. Biashara inapokatiwa bima, wakala wa bima atafidia hasara itakayotokea iwapo biashara itakumbwa na majanga.

Bima ni kitu pekee kitakachoiweka biashara yako katika njia ya usalama zaidi. Unapomiliki bima unajihakikishia usalama wako na wa biashara yako kwa sababu bima zimegawanyika katika aina mbalimbali kama zilivyoainishwa hapa chini:

Aina za Bima:

Bima ya Wizi

Aina hii ya bima inahusisha kulipa fidia kwa madhara yanayoweza kutokea baada ya wizi wa mali za biashara.

Bima ya Moto

Hii mtu anaweza kulipia bima ya nyumba na vifaa vyake vya biashara dhidi ya moto.

Majanga ya asili

Hii inahusu kulipia biashara kutokana na madhara yanayotokana na majanga ya asili kama vile mafuriko na tetemeko.

Mpango wa Bima ya Afya/Matibabu

Aina hii ya bima inaweza kuwa katika aina mbili zifuatazo:

Aina ya kwanza ya bima ya afya ni kutoa huduma ya afya kwa watu. Katika aina hii ya bima, watu wanaweza kupata huduma za afya baada ya kujiunga na mpango wa bima ya afya.

Aina ya pili ya bima ya afya ni kulipia fidia kutokana na madhara ya aina yoyote yanayoweza kutokea kutokana na ajali au kifo wakati wa kazi au katika mazingira ya kazi.

Bima ya mali

Katika aina hii ya bima mtu alipie bima ya mali. Kuna aina nyingi zinazoweza kulipiwa bima kama zifuatazo:

Mizigo ya bandari: Hii inahusisha kinga dhidi ya upotevu wa mizigo wakati inasafirishwa baharini (kwa meli), angani (kwa ndege) au ardhini (kwa barabara au reli).

Magari: Sheria inataka magari yote katika barabara za umma kuwa na bima au kinga dhidi ya dhima kwa kuumia  kwa abiria na upotevu wa mizigo.

Faida za Bima ya Afya

  1. Usalama dhidi ya matukio yasiyotarajiwa kama vile wizi na moto- Bima inasaidia kumhakikishia mfanyabiashara usalama na ulinzi wa biashara yake.
  2. Mfanyabiashara anaweza lipia bima biashara yake ili asidhurike na madhara kama vile wizi na moto. Kwa maana hiyo, mhusika hupata fidia yote baada ya kutokea tukio hilo.
  3. Njia rahisi za fidia ya hasara endapo bahati mbaya inakutokea- Bima imekuwa ikisaidia wafanyabiashara wengi kurudi katika biashara zao haraka pale inapotokea kwa bahati mbaya wakapatwa na majanga kama vile moto, mafuriko na tetemeko.
  4. Mtu anaweza lipia bima ya biashara yake ili asidhurike hasara ikitokea. Kama biashara imelipiwa bima, baadhi ya hasara zaweza kulipwa/kufidiwa na hivyo kuwezesha kuendelea kuwepo wa biashara husika.
  5. Bima yatoa fursa katika huduma bila kulipia fedha halisi kwa wakati husika, kwa mfano, bima ya afya. Hii ni kwa ajili ya aina zingine za bima kama vile bima ya afya. Mtu hupata fursa kamili kwa ajili ya huduma za afya bila kulipa hata senti. Hapa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wanaweza kuwa na uhakika wa usalama kwa afya zao na za familia zao pindi wanapougua.

Sheria inasema nini kuhusu Bima?

Sheria ya Bima ya Mwaka 2009

Sheria iliyoanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Nchini (Tanzania Insurance Regulatory Authority). Chini ya Sheria hii, mamlaka imepewa nguvu ya kuongoza na kusimamia biashara ya bima na masuala yote yanayohusiana na bima Tanzania Bara na Zanzibar. Sheria hii inaipa mamlaka nguvu ya kusimamia na kuratibu shughuli zote za bima. Sheria hii inaainisha kanuni za maadili kwa ajili ya bima na taarifa zote muhimu za kuendesha biashara ya bima, wakati mamlaka ya usajili wa biashara za bima amepewa Kamishna wa Bima au Naibu Kamishna wa Bima.

Sheria hii inaelekeza kwamba, mtu yoyote atakayeanzisha biashara ya bima lazima awe mkazi wa Tanzania, lakini kama ni kundi angalau theluthi moja ya wajumbe wa bodi wawe ni wakazi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria inaelekeza taratibu na nyaraka muhimu za kuanzisha biashara ya bima. Pia inaelekeza haki ya bima ya tatu kama vile kuwa na bima dhidi ya dhima kama kufilisika pamoja na haki ya kupata taarifa kwa mwendesha biashara ya bima.

Kanuni za Bima Ndogo za Mwaka 2003

Kanuni hizi zinahusu wakala wa bima ndogo na mwekeza bima anayehusika na bima kwa ujumla kuhusu bima ndogo ya mali au ya maisha. Huduma chini ya kanuni hizi zinahusu banda, mifugo, vifaa vya uvuvi, mazao ya kilimo, zana za biashara ndogo au vifaa au ajali ya mtu binafsi au kundi, elimu, muda wa mkopo, maisha ya familia na bima ya mkataba wa mazishi.

Licha ya kuwepo huduma hizi za utoaji bima katika nchi za Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla bado zipo changamoto mbalimbali zinazokwamisha

  1. Ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya bima- Elimu kuhusu bima imekuwa ikitolewa maeneo ya mijini tu lakini wakazi wengi wa vijijini hawana elimu ya kutosha kuhusu bima. Wengi wanajua bima ya afya.
  2. Watu kutokuwa na mwamko kuhusu bima- Idadi kubwa ya watanzania hasa walioko vijijini hawajapata mwamko wa kutosha kuhusiana na bima kutokana na ukosefu wa semina, warsha na makongamano yanayohamasisha watu kujiunga na bima mbalimbali ikiwemo bima za biashara.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter