Wataalamu wa bima ya maisha wanaamini kuwa wakala wa bima hawajafanya kazi yao ipasavyo ya kuwaelimisha wananchi juu ya bima hiyo muhimu badala yake wamejikita katika aina nyingine za huduma hiyo.
Katika mkutano wa mwaka wa Umoja wa Chama cha Mawakala wa Bima Tanzania, Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Dk Mussa Juma amesema mawakala nchini wanatakiwa waipe uzito biashara ya bima ya maisha kwani kwani soko lake bado halijaguswa ipasavyo.
Dk Juma alisema mawakala wengi nchini wamejikita katika bima za magari na kusahau bima ya maisha ambayo ina maslahi makubwa.
“Kimsingi kila mtanzania anatakiwa awe na bima ya maisha,” alisema.