Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 66 mwaka jana.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu walikuwa milioni 35.3 hadi mwezi Desemba mwaka jana sawa na asilimia 61 ya watu wote nchini.
Dk Nchemba amesema hayo wakati akifungua mkutano wa 10 ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Jumuiya ya Kimataifa ya Huduma Jumuishi za Fedha (AFI) ulioshirikisha viongozi wa jumuiya ya ukanda wa Afrika (AfPI) jijini Arusha, Juni 23, 2022.
“Kuanzishwa kwa huduma hizi za kifedha kwa njia ya simu, pamoja na huduma za benki kwa wakala na benki kwa njia ya simu, kuliongeza upatikanaji wa huduma za kifedha nchini ikiwa ni pamoja na maeneo ya vijijini,” amesema.Miamala ya fedha