Home FEDHAMIKOPO Masharti muhimu ya mikopo benki

Masharti muhimu ya mikopo benki

0 comments 321 views

Kukopa ni jambo la kawaida katika maisha ya kila siku. Usione aibu kukopa ili mradi uwe na uhakika wa kulipa mkopo huo. Kuna milionea mmoja hapa nchini aliwahi kusema kuwa mtu yeyote hawezi kupata mafanikio ya kiuchumi bila kukopa hivyo basi hakikisha una malengo na mkopo huo ili utakapokuwa unahitajika kulipa uwe unafahamu ni wapi fedha hizo zitatoka. Benki nyingi nchini zimekuwa zikizindua aina mbalimbali za mikopo kila siku ili kuwasaidia wananchi kujipatia maendeleo na kuchangia katika pato la taifa.

Yafuatayo ni baadhi ya masharti ambayo benki nyingi hutoa kwa mkopaji.

  1. Historia ya kukopa, hakuna benki itakayokupatia mkopo kama una historia ya kukopa na kutorejesha hivyo kama unahitaji mkopo au unategemea kupata mkopo inabidi uwe na historia nzuri ya mikopo. Ukiwa mkopaji na mrudishaji mzuri, utaweza kukopa zaidi na zaidi.
  2. Kila benki huuliza kama unakopa kwa ajili ya kuanzisha sehemu ya kujipatia kipato au kama una eneo/biashara endelevu ambayo inaweza kukusaidia baadae kulipa mkopo huo. Kama huna sehemu ya kupata kipato, inakuwa ngumu kupata mkopo ingawa unaweza kuweka vitu kama nyumba au kiwanja ili kupewa mkopo. Hii inaweza kuleta changamoto hasa pale ukishindwa kulipa mkopo huo kwani benki italazimika kuchukua mali zako. Unashauriwa kuwa na eneo au shughuli inayokuingizia fedha kabla ya kuchukua mkopo.
  3. Ili kukopa benki, mkopaji anatakiwa kuwa na mdhamini ambaye ikitokea mkopaji ameshindwa kulipa mkopo, basi inakuwa ni wajibu wa mdhamini kuhakikisha mkopo huo unarudishwa aidha kwa kulipa yeye au kumsisitiza mkopaji kulipa.
  4. Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN). Hii huwahakikishia kuwa una shughuli ambayo unafanya na unalipa kodi serikalini.
  5. Unatakiwa kuwa na kitambulisho na barua kutoka serikali ya mtaani kwako.

Kuna benki nyingine huwa na masharti zaidi ya haya, unachotakiwa kufahamu ni kwamba taasisi za fedha huweka masharti hayo sio kwa lengo la kumkomoa mkopaji, bali huweka masharti hayo kwa ajili ya kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika bila changamoto zozote.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!