Home FEDHA Serikali kulipa madeni ya watumishi

Serikali kulipa madeni ya watumishi

0 comment 147 views

 

Na Mwandishi wetu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  amesema baada ya kumalizika kwa zoezi la kubaini watumishi hewa,serikali italipa madeni yote ambayo yamehakikiwa na kubainika kuwa ni halali. Amesema pia watumishi katika taasisi zote wahudumie wananchi na kufanya kazi kwa bidii.

Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Majaliwa ameongeza kuwa Rais Magufuli alisitisha malipo hayo  ili kupisha zoezi la kubaini watumishi hewa.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa, serikali kwa sasa inadhibiti madeni mapya na kwamba kila mtu ana uhuru wa kujiendeleza kitaaluma lakini ni lazima awasilishe barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri. Maombi hayo yakikamilika ndipo muombaji ayawasilishe chuoni.

Waziri Majaliwa pia amesema serikali imefuta utaratibu wa Mtumishi kuandika barua ya kupandishwa daraja au cheo ili kupata malipo mapya huku akitoa onyo kwa wapokea rushwa na watumishi wasio waadilifu kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao mara moja.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter