Home FEDHA Wateja wa Tigo kufaidika na gawio

Wateja wa Tigo kufaidika na gawio

0 comment 109 views

Wateja na watumiaji wa huduma za Tigopesa wanatarajia kupata gawio la Sh.2.35 bilioni katika awamu ya pili ya mgao huo iliyoishia Juni mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Simon Karikari ambaye ameeleza kuwa, wateja milioni 7 kati ya milioni 12 ndio wanaotumia huduma ya Tigopesa na ndio watakaofaidika kupitia huduma hiyo ambayo imetajwa kusambaa nchi nzima ikitoa huduma kwa wafanyabiashara takribani 40,000 pamoja na mawakala wapatao 85,000.

Soma Pia TIGO yatumia milioni 18 kumaliza tatizo la maji

Akielezea mchanganuo wa utoaji wa riba kwa wateja wake, Karikari amesema kuwa tangu mwaka 2014 kampuni ya Tigo imekuwa ikitoa gawio la riba  kwa wateja wake wa huduma za fedha (Tigopesa) ambapo mpaka sasa kampuni hiyo imeweza kutoa kiasi cha Sh. 81.8 bilioni na kuongeza kuwa kiwango anachopata mteja kama gawio hutegemea na kiasi cha fedha kilichopo katika akaunti ya mteja lakini pia kanuni za Benki kuu ya Tanzania zimekuwa zikizingatiwa.

Soma Pia Mambo ya kuzingatia unapoanzisha biashara mtandaoni

Aidha Mkurugenzi huyo ameeleza kuhusu huduma mpya ya Tigo inayomsaidia mteja kuwa na uwezo wa kusitisha muamala wa fedha iliyotumwa kimakosa kwenda kwa mteja mwingine na kueleza kuwa huduma hii itasaidia kuwarahisishia wateja wao usalama wa fedha zao pale zinapotumwa kimakosa huku huduma hiyo ikiambatanishwa na huduma ya teknolojia ya Masterpass QR yenye kuwawezesha wateja wa Tigopesa wanaomiliki Mastercard na Visa kufanya malipo na manunuzi ya bidhaa na huduma.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter