Biashara EAC juu

0 comment 107 views

Biashara kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeendelea kukua na kupandisha mauzo kutoka Dola za Marekani 1.5 bilioni mwaka 2015 hadi Dola 5.5 bilioni mwaka 2017, ikiwa ni ongezeko la Dola bilioni nne za Marekani ambazo ni sawa na takribani trilioni 8.4 za Tanzania. Moja kati ya vitu vilivyotajwa kuchangia ukuaji huo ni kuimarika kwa mtangamano ndani ya jumuiya, hivyo kukuza ushirikiano katika sekta mbalimbali zikiwemo za biashara na masoko.

Mkurugenzi Mtendaji wa Forodha na Biashara wa EAC, Kenneth Bagamuhunda amesema japokuwa itachukua muda kuufikia mtangamano kamili, tayari matunda ya kuanzishwa kwa Umoja wa Forodha ndani ya jumuiya mwaka 2005 yameanza kuonekana mapema.

“Tangu Januari 2005, mtangamano katika biashara ndani ya EAC umekuwa na mafanikio makubwa. Mwaka 2005, biashara baina ya mataifa ndani ya jumuiya zilikuwa Dola bilioni 1.5, lakini kufikia mwaka 2017, tunazungumzia dola bilioni 5.5”. Amefafanua Bagamuhunda.

Aidha katika maelezo yake, Mkurugenzi huyo amesema kwa kiasi kukubwa, uimarishwaji wa sekta ya miundombinu umerahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine na hivyo kukuza biashara.

“Mkazo upo katika kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, huku ndiko tunakoamini kutachangia ukuaji wa kiuchumi ndani ya jumuiya. Tunapambana pia kupunguza vikwazo vya biashara katika nchi wanachama”. Ameeleza Bagamuhunda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter