Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kukutana na zaidi ya wanawake 10,000 wa mkoa wa Dodoma kesho June 08, 2021.
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka imesema Rais Samia ataongea na wanawake wa mkoa huo kwa niaba ya wanawake wote nchini katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.
Mtaka amesema wanawake kutoka katika makundi mbalimbali katika wilaya za mkoa huo wamealikwa.
“Kwa uchache pia kama makundi ya wabunge wanawake bila kujali uko chama gani, madiwani na makundi kama wajasiriamali, mama ntilie na kila aina ya wanawake watapata nafasi ya kuwakilishwa na wenzao,” amesema.